Savvy FM
Savvy FM
July 18, 2025, 2:47 pm

Wakulima wa Kijiji cha Kivul, kitongoji cha Olmatejo jijini Arusha, wameiomba serikali kuwasaidia kuboresha miundombinu ya kilimo hasa ya maji ya umwagiliaji ambayo imekuwa changamoto kubwa kutokana na mvua.
Na Jenipha Lazaro
Wakizungumza wakati wa zoezi la kurekebisha mifereji na mabomba ya maji kwa ajili ya kilimo, wamesema kuwa mmonyoko wa udongo kwenye mto unaotenganisha vitongoji hivyo umeharibu miundombinu iliyokuwepo na kuzuia maji kufika upande wa pili wa mashamba yao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Peter Elias, amesema licha ya baadhi ya mamlaka kufahamu hali hiyo, bado hawajapata msaada wowote, jambo linalohatarisha usalama wa watoto wanaotumia maeneo hayo kuvuka mto.