Savvy FM
Savvy FM
July 12, 2025, 10:57 am

Wanawake nchini wametakiwa kuacha hofu na kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Urais, ubunge na udiwani.
Na Mariam Mallya
Kiongozi wa Act Wazalendo ambaye pia ametia nia ya kugombea nafasi ya Urais kwa tiketi ya chama hicho Doroth Semu ameyasema hayo wakati akiwa katika studio za Savvy FM ambapo amesema wanawake wanaweza hivyo wajitokeze kuchukua fomu.
Doroth amesema moja ya sera ya Act Wazalendo ni 50-50 hivyo wanamtazama mwanamke kama mtu ambaye anaweza kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo katika nchi .
Kiongozi huyo wa Act Wazalendo amesema chama hicho kimejidhati kuweka wagombea bora kwenye nafasi zote na kuhakikisha wanaweka ilani bora itakayojibu changamoto za wananchi.