Savvy FM
Savvy FM
July 3, 2025, 8:08 pm

Wazazi washauriwa kutokuwaficha watoto wenye ulemavu na badala yake wawape nafasi ya kupata elimu kwani wanahaki kama watoto wengine.
Na Mariam Mallya
Mwalimu wa Shule ya Msingi Uhuru iliyopo mkoani Arusha, Glory Urio akizungumza na Savvy Fm Mwalimu Urio amasema shule hiyo ina kitengo maalumu cha watoto wenye ulemavu wa akili pamoja na usonji kinachowapa fursa watoto hao kupata elimu na kujifunza haki zao.
Mwalimu Urio amesema zipo changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika kitengo hicho maalumu ikiwemo wazazi kuwakimbia watoto wenye ulemavu na kuwatelekeza.
Pamoja na hayo ameishauri jamii kulinda haki za watoto ikiwemo kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatilii.
Kwa upande wake Hassan Imran ambaye ni mzazi amesema Wazazi wametakiwa kupewa elimu ili waweze kuondokana na mawazo hasi yanayopelekea kuwaficha watoto wenye ulemavu.