Savvy FM
Savvy FM
June 19, 2025, 2:38 pm

“Wafugaji tujiwekeze kwenye elimu wenzetu wanaenda juu sisi tunarudi chini lazima tusome ufugaji unahitaji elimu”
Na Mariam Mallya
Diwani wa kata ya Endamily wilayani Mbulu katika mkoa wa Manyara na Mwenyekiti wa Bajuta International (T) Ltd, Gesso Bajuta amewataka vijana wa jamii ya kifugaji wilayani Longido mkoani Arusha kuwekeza kwenye elimu kwani ufugaji wa sasa unahitaji elimu zaidi.
Hayo ameyasema wakati akiwa katika Sherehe za mila ya Kimaasai la kubariki rika la Irmegolik nakusema kuwa pamoja nakuwa Morani vijana wanapaswa kwenda shule kwani serikali imejenga shule kwa ajili ya wananchi.
Diwani huyo ambaye pia ni mfugaji wa jamii ya Wadatoga, Bajuta amewataka wafugaji kufuga kisasa kulingana na mazingira.