Savvy FM
Savvy FM
June 10, 2025, 6:46 pm

Walimu wote nchini watakiwa kufundisha kwa weledi nakujua kuwa watanzania wana matarajio makubwa kutoka kwako katika kuleta mapinduzi makubwa ya kimaendeleo katika sekta ya elimu
Na Mariam Mallya
Naibu Waziri wa Tamisemi anayeshughulikia elimu, Zainab Katimba amesema hayo wakati akizindua awamu ya pili ya ugawaji wa vifaa vya TEHAMA kwa shule za sekondari katika shule ya sekondari ya Arusha nakusema kuwa walimu wanapaswa kujituma na kuhakikisha sera ya elimu inafanyika kwa vitendo.
Naibu Waziri Zainab Katimba amesema serikali inaamini kuwa matumizi ya TEHAMA mashuleni yataleta mapinduzi makubwa kwani walimu wataongeza ufanisi katika ufundishaji na wanafunzi watapata maarifa ya ziada.
Aidha amesema mpaka sasa awamu ya kwanza ya ugawaji wa vifaa vya TEHAMA umeshafanyika kwa shule 231 na sasa ni awamu ya pili ya ugawaji wa vifaa hivyo ambapo vitanufaisha shule 422.