Savvy FM

Jamii yatakiwa kupinga ukatili

June 5, 2025, 2:58 pm

Mkurugenzi Mtendaji shirika la Voice of Women Africa, Veronica Kidemi akizungumza katika studio za Savvy FM. Picha na Fredrick Lyimo

Wananchi watakiwa kuungana na kuwa mstari wa mbele kukemea na kupinga ukatili katika jamii.

Na Mariam Mallya

Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Voice of Women Africa lililopo mkoani Arusha, Veronica Daudi Kidemi amesema kuwa jamii ina nafasi kubwa ya kupinga vitendo vya kikatili kwa kutoa taarifa pindi wanapoona matendo maovu yakifanyika katika jamii.

Bi Veronica ameyasema hayo wakati akizungumza katika studio za Savvy FM nakusema kuwa jamii bila ukatilii inawezekana.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Voice of Women Africa Veronica Daudi Kidemi

Aidha Bi. Kidemi amewataka wanawake kusimama kwenye nafasi zao na kuvunja ukimya na kutokuvumilia ukatilii ndani ya ndoa, nakusema kulingana na taarifa ya Tathmini ya Ukatili wa Kijinsia Tanzania iliyoandaliwa na Benki ya Dunia mwaka 2022, 40% ya wanawake wote wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili na 17% wamepitia ukatili wa kingono.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Voice of Women Africa Veronica Daudi Kidemi

Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo amewakaribisha watu wenye uhitaji wa mikono bandia kujitokeza tarehe 11 -14 mwezi wa saba mwaka huu katika hospitali ya mkoa wa Arusha Mount Meru ili kupatiwa mikono hiyo bure.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Voice of Women Africa Veronica Daudi Kidemi