Savvy FM

Milioni 5.3 kukarabati kituo cha afya Engorora

April 24, 2025, 10:16 am

Wananchi wa kijiji cha Engorora wakiwa kwenye mkutano. Picha na Aloyce Mkufya

Halmashauri ya Arusha imetenga kiasi cha shilingi milioni 5.3 kwa ajili ya ukarabati wa jengo la zahanati ya Kijiji cha Engorora ambalo limekuwa likikabiliwa na nyufa kwa muda mrefu hali inayosababisha kituo hicho kutotoa huduma za usiku kutokana na wahudumu kuhofia  jengo hilo kuanguka muda wowote.

Na Aloyce Mkufya

Katika changamoto tatu tulizoziibua mwaka jana katika kituo cha afya Engorora ambazo ni ubovu wa jengo la kituo ,kutomalizika ujenzi wa nyumba ya watumishi pamoja na barabara ya kwenda kituoni kuwa mbovu tayari baadhi ya changamoto zimeanza kutatuliwa ikiwemo ukarabati wa kituo cha afya cha Engorora ambapo niliwakuta mafundi wakiendelea kukarabati jengo hilo.