Radio Kwizera
Radio Kwizera
August 4, 2025, 6:54 pm

Wasimamizi wanatakiwa kufuata sheria, taratibu na miongozo ya Tume Huru ya Uchaguzi kwa kushirikisha vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili katika hatua zote kuepuka migogoro
Na Shafiru Athuman- Muleba, Kagera
Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata Wilayani Muleba Mkoani Kagera wametakiwa kufanya utambuzi wa vituo vya kupigia kura kubaini mahitaji maalum ya vituo husika ili uchaguzi ufanyike kwa uhuru na amani.

Hayo yameelezwa leo hii na Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Muleba Kusini na Muleba Kaskazini Bw. Yona Chalugamba wakati ufunguzi wa mafunzo kwa wasimaizi wasaidizi wa uchaguzi 86 ngazi ya kata.
Bw. Chalugamba amesema kuwa wasimamizi wanatakiwa kufuata sheria, taratibu na miongozo ya tume huru ya uchaguzi kwa kushirikisha vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili katika hatua zote kuepuka migogoro ili uchaguzi ufanyike uhuru na amani.
Aidha mafunzo hayo yameambatana na kiapo cha kutunza siri za usimamizi wa uchaguzi kiapo cha kujitoa uanachama wa chama chochote cha siasa kilichotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu na Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Muleba Daniel Nyamkerya.
