Radio Kwizera
Radio Kwizera
June 28, 2025, 12:35 pm

Amewataka vijana, wanawake na makundi mengine kuendelea kuonyesha uwezo wao serikalini hasa baada ya kupata nafasi za juu za maamuzi.
Na Samwel Masunzu- Geita
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Kata ya Nyachiluluma wilayani Geita mkoani Geita Bi. Esther James ametangaza nia ya kuwania Ubunge katika jimbo la Katoro wilayani Geita mkoani humo.
Akizungumza mjini Geita Bi. Esther James amesema lengo la kutia nia ni kuonyesha nguvu ya wanawake katika uwakilishi badala ya kusubiri nafasi za viti maalumu.
Amesema anaamini wanawake wana uwezo wa kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo kama ilivyo kwa wanaume.
Aidha amewataka vijana, wanawake na makundi mengine kuendelea kuonyesha uwezo wao serikalini hasa baada ya kupata nafasi za juu za maamuzi.

Jimbo la Katoro ni moja ya majimbo ambayo yamekatwa hivi karibuni ambapo jimbo hilo limegawanywa kutoka jimbo la Busanda.