Radio Kwizera

Raia wa Burundi afia kwenye gari la abiria Ngara

May 13, 2021, 5:24 pm

Na; Asma Ahmed

Watu wawili wanaosadikiwa kuwa Raia wa Burundi wamekutwa wakiwa wamefariki katika matukio tofauti Wilayani Ngara Mkoani Kagera

Mkuu wa jeshi la Polisi wilayani Ngara Bw Abeid Maige amesema tukio la kwanza limetokea jana kwenye Kitongoji cha Mumasama ambapo mwili wa kijana ambaye hajafahamika umekutwa umetelekezwa kwenye uwanja wa Kokoto mjini Ngara

Amsema katika tukio la pili ambalo pia limetokea jana, Bw Pascal Rulidikiye aliyekuwa akisafiri kutoka Karagwe kwenda nchini kwao Burundi amefariki akiwa ndani ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace na hali hiyo imegunduliwa na dereva wa gari hilo baada ya kufika Benaco wilayani Ngara

Sauti ya OCD Ngara Abeid Maige

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Ngara, Nyamiaga Dr David Mapunda amesema kwa nyakati tofauti wamepokea miili ya marehemu hao na kwamba hadi sasa hakuna ndugu aliyejitokeza kwa ajili ya kutambua miili hiyo SEO paslaugų kaina https://seopaslaugos.com/seo-kaina/

Sauti ya Mganga Mfawidhi Hospitali ya Nyamiaga Dr David Mapunda
Mganga Mfawidhi Wilaya ya Ngara Dr David Mapunda