Mlipuko wa Corona uliathiri Soko la Kahawa Ngara
May 7, 2021, 7:01 pm
Na; Seif Upupu
Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Kahawa, Ngara Farmers Cooperative Society cha wilayani Ngara mkoani Kagera kimesema kuwa mlipuko wa Virusi vya Corona duniani uliathiri Soko la Kahawa kutoka kwa wakulima wilayani humo
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama hicho Bw David Bukozo amesema kuwa kufuatia mlipuko wa Covid-19 umesababisha wauze Kahawa kwa bei isiyotarajiwa licha ya kuwa kulikuwa na Kahawa safi ya kutosha
Bw Bukozo amesema kuwa ili kuhakikisha wakulima wanazalisha kwa tija, Chama hicho kiko mbioni kuandaa mafunzo kwa wakulima ili kuwawezesha kulima kisasa na kwamba mafunzo hayo yanatarajiwa kuanza kutolewa kabla ya mwezi June mwaka huu
Katika hatua nyingine Bw Bukozo amesema kuwa Chama hicho kinajiandaa kulipa malipo ya pili kwa wakulima wa Kahawa na kwamba kilo moja italipwa kwa Sh 30 kwa wote waliopeleka Kahawa yao kwenye Chama hicho