Wakulima 120 Ngara, kunufaika na Mafunzo ya Kilimo hai endelevu
May 3, 2021, 7:58 pm
Na; Marco Pastory
Jumla ya wakulima 120 wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya awali ya kilimo hai endelevu kwa mazao manne katika vijiji vitano vya wilaya Ngara Mkoani Kagera
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika kijiji cha Kasulo Wilayani Ngara yameazimia kutoa elimu ya kilimo kwa mazao ya Nanasi, Parachichi, Migomba na Kahawa yaliyotolewa na Shirika la Marafiki wa Afrika Tanzania (MAT)
Mafunzo hayo yameanza leo kwa wakulima 24 kutoka kijiji cha Kasulo kata ya Kasulo na yataendelea kutolewa kwa vijiji vingine vilivyosalia na kukamilisha idadi ya jumla ya wakulima 120 wanaotarajiwa kufikiwa na mafunzo hayo
Mwandishi wa Radio Kwizera Marco Pastory amefanya mahojiano na Mratibu wa Mafunzo hayo Bw Mushabe Willy ambaye amesema mafunzo hayo ya awali yamewahusisha wakulima kutoka vijiji vya Kasulo, Mshikamano, Bugarama, Mugoma na Rulenge