Tembo wavamia mashamba Ngara
April 2, 2021, 12:28 pm
Na; Felix Baitu.
Zaidi ya Ekari 5 za mazao mbalimbali kwenye kijiji cha Lwakaremela kata ya Kasulo wilayani Ngara mkoani Kagera zimeharibiwa na Tembo waliovamia kijiji hicho wakitokea katika hifadhi ya wanyapori ya Burigi Chato
Wakazi wa kijiji hicho wamesema Tembo hao wameharibu mazao yakiwemo Maharage na Migomba na kusababisha hofu kwa watoto kwa kuwa wanashindwa kwenda shule kwa wakati wakihofia usalama wao.
Wamesema tangu March 6 mwaka huu, Tembo hao wamekuwa wakivamia mashamba kila siku kuanzia majira ya saa Moja usiku na kuondoka saa kumi na moja alfajiri
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw Aidan Bahama amesema kijiji cha Lwakaremela ni Shoroba ama njia ya Tembo na kwamba tatizo hilo limekuwa likijitokeza kila mwaka na tayari wametoa elimu ya namna ya kujilinda kwa kuwa hadi sasa hakuna suluhisho la kudumu.
Tangu kuanza kwa mwaka huu, hii ni mara ya 3 Tembo hao kuingia kijijini humo ambapo mwezi Januari waliingia Tembo 60 na mwezi February wameingia zaidi ya Tembo mia moja