Wazee walalamika kutoshirikishwa kwenye vikao vya kijiji na kata Kasharunga, Muleba.
March 31, 2021, 8:58 pm
Na; Shafiru Asumani
Baadhi ya wazee wa Kijiji Cha Kyamworwa kata ya Kasharunga Wilayani Muleba Mkoani Kagera wamelalamikia kitendo cha kutoshirikishwa kwenye vikao vya maendeleo ya vijiji na kata ambavyo vinaweza kuwasilisha kero mbalimbali zinazowakabili.
Wazee hao wamesema hayo kwenye mkutano Mkuu uliofanyika katika Kijiji hicho ambapo wamesema kuwa wazee hao Wana kero mbalimbali lakini wamekuwa hawashirikishwi hivyo wameomba viongozi husika kuweza kuwashirikisha kwa mujibu wa sheria.
Naye Katibu wa balaza la wazee kijiji hicho cha Kyamworwa Shekh Anas Mshumbuzi amesema bado kuna chagamoto ya baadhi ya wazee kuchagishwa michango ya maendeleo kwa lazima kutokana baadhi yao hawana uwezo wa kufanya kazi.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kasharunga Bw. Theobard Kulandebe ambaye alikuwa mgeni Rasmi kwenye kikao hicho amesema tangu aingie madarakani ameitisha kikao mara moja hivyo atahakikisha anashirikiana na wazee hao ili waweze kupata haki zao pindi wanapokuwa wanaudhuria kwenye vikao hivyo vya maendeleo.