Buha FM Radio
Buha FM Radio
May 17, 2025, 2:15 pm

Shirika la Meremeta chini ya Mkurugenzi wake Ndg. Justine Damiano Mbizi limesema linawasaidia kuwainua kiuchumi watoto wa kike waliopata ujauzito wakiwa shuleni kwa kuwapatia mitaji pamoja na kuwarudisha shuleni pale inapowezekana.
Na: Sharifat Shinji
Mkurugezi wa shirika la Meremeta Mkoa wa Kigoma Ndg. Justine Damiano Mbizi amesema kuanzia mwaka 2022 hadi 2024 wamewafikia watoto wa kike zaidi ya 1,000 walioacha shule kwa sababu mbalimbali ikiwemo kubeba ujauzito wakiwa shuleni.
Ameyabainisha hayo wakati wa mahojiano ya moja kwa moja katika studio za Buha FM radio huku akiwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kushirikiana na taasisi hiyo ili kuwaokoa na kuwasaidia watoto wa kike katika kutimiza ndoto zao.
Kwa mujibu wa chapisho la jarida la Wanahabari Wananawake Tanzania TAMWA lililochapishwa mwaka 2017 walichapisha kuwa “hali ya mtoto wa kike kukosa elimu huchagiza
mimba za utotoni, ndoa za utotoni na ongezeko la unyanyasaji kwa watoto kike.
Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 inaeleza kwamba ni jukumu la mzazi, mlezi au mtu
yeyote anayeishi na mtoto kumpa haki ya elimu na kujifunza”