Vwawa FM Radio

Kodi zahatarisha biashara mpaka wa Tunduma

August 16, 2025, 12:59 pm

Picha ya wadau mbalimbali wakishiriki kwenye jukwaa maalum la wafanyabiashara na taasisi za kifedha lililoandaliwa na Benki ya NMB. Picha na John Kiango

Wafanyabiashara Tunduma waomba serikali kuboresha mfumo wa kodi mpakani ili kurahisisha biashara na kuongeza ushindani.

Na Emmanuel Mkondya

Wafanyabishara wa Tunduma wameiomba kuweka mifumo rafiki ya kodi katika  mpaka wa Tanzania na Zambia ili waweze kunufaika na bishara ya mpakani

wamesema hayo  Agosti 13 Mwaka huu, kwenye jukwaa maalum la wafanyabiara na Taasisi za kifedha ya NMB benki lililofanyika katika ukumbi wa Ukinga Hill katika halmashauri ya Mji wa Tunduma Wilayani Momba.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara katika Mji wa Tunduma Nyalu Mifwa amesema mifumo ya Kodi ya nchi ya Tanzania sio rafiki kwa wafanyabiashara hali iliyosabanisha baadhi yao kurazimika kuhamia nchi jirani ya Zambia ambako kodi za Zambia  zinajumuisha kodi zote wakati Tanzania kila sekta ina kodi yake na kuomba serikali kuona namna ya kurekebisha mfumo huo.

Sauti ya Mwenyekiti wa wafanyabiashara katika Mji wa Tunduma Nyalu Mifwa

Akibu hoja hiyo Mkuu wa idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Songwe Paulo Mhache serikali  inaendelea kufanya mazungumzo ya kuweka mazingira mazuri na rafiki ya kibiashara mpakani ili kunufaisha pande zote mbili za nchi.

Sauti ya Mkuu wa idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Songwe Paulo Mhache

Kwa upande Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu, Wagofya Mfalamagoha, amesema jukwaa hilo limekusudia kuwaunganisha wafanyabiashara na wadau muhimu kwa pamoja ili kujadili na kutatua changamoto zinazokwamisha shughuli zao za kibiashara.