Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
June 5, 2025, 4:36 pm

Ni kuhusu umiliki wa zawadi ya ardhi au gari
Na Pili Mwang’osi
Vijana wanaotarajia kuoa ama kuolewa wametakiwa kutambua kuwa zawadi wanazopewa kwenye sherehe ni hazina ya wanandoa wote.
Mchungaji wa Kanisa la Moravian,Ushirika wa Isangu, Tabson Mgala maarufu Walola Bwana, amesema hayo alipozungumza na Vwawa Fm iliyotaka kujua maoni yake kuhusu zawadi hizo.
Vwawa Fm imeomba maoni ya mchungaji huyo baada ya kuwepo kwa mkanganyiko wa nani anamiliki kati ya mume na mke.
Amesema zawadi za mali yakiwemo mashamba, nyumba na Magari yanayotolewa zawadi wakati wa sherehe za kumuaga binti ( send off) au harusi yenyewe.
Mchungaji Walola Bwana amesema kijana wakiume na wa kike wakifunga ndoa mali zote zitamilikiwa na wote, haijalishi uwezo wao binafsi na kwamba kama mmoja wao atafariki, wazazi hawana mamlaka ya kuingilia mali Hizo.
Aidha amesema wazazi wanapotoa zawadi kwa binti yao hawapaswi kuzidai kwani mali hizo zinabaki kwa wanandoa husika.
Lakini Mwanasheria, Lusungu Ndawala wa Mbozi amesema binti anapopewa zawadi za mali au kimiliki kama vile uwanja, nyumba au gari anayo mamlaka ya kuandika umiliki wa mali hizo.
sauti ya Mwanasheria, Lusungu Ndawala
Baadhi ya wazazi mjini Vwawa akiwemo Anangisye Kamendu, wametoa maoni yao kuhusu suala hilo.