Vwawa FM Radio

Biashara zavurugika Isongole kufuatia kufungwa kwa mpaka wa Malawi

May 26, 2025, 12:37 pm

Mpaka wa Tanzania na Malawi.Picha na Kennedy Sichone

Kufungwa kwa mpaka wa Isongole imekuwa kilio kwa wafanyabiashara wa mpakani hususani wanaouza mazao nje ya nchi

Na Kennedy Sichone

Wafanyabiashara wa Isongole na maeneo ya jirani katika Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe, April 28 mwaka huu wameiomba serikali kufungua tena mpaka kati ya Tanzania na Malawi ili waweze kuendelea na shughuli zao za kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

Ombi hilo limekuja kufuatia hatua ya Serikali ya Malawi kufunga mpaka huo tangu mwezi Machi mwaka huu, kwa lengo la kuzuia uingizaji wa bidhaa za kilimo kutoka Tanzania. Hatua hiyo imeathiri kwa kiasi kikubwa biashara ya mazao na kusababisha usumbufu kwa wakulima na wafanyabiashara wa pande zote mbili.

Awali, Waziri wa Kilimo wa Tanzania, Hussein Bashe, alitangaza kuwa serikali itachukua hatua kali dhidi ya nchi ya Malawi pamoja na Afrika Kusini, akieleza kuwa vikwazo hivyo vya kibiashara vinakiuka makubaliano ya kibiashara ya kikanda na kuathiri uchumi wa wakulima wa Kitanzania.

Baadhi ya wafanyabiashara waliotoa maoni yao wamesema kuwa kufungwa kwa mpaka huo kumeathiri vibaya mapato yao, huku wakitoa wito kwa serikali za pande zote mbili kutafuta suluhu ya haraka ili kurejesha hali ya kawaida ya biashara.

Sauti ya wafanyabiashara ya mazao