Vwawa FM Radio
Vwawa FM Radio
April 24, 2025, 9:06 am

Waendesha bodaboda wanatajwa kuvujisha siri za wateja wao
Na Mkaisa Mrisho
MBOZI
Baadhi ya watumiaji wa vyombo vya usafiri maarufu kama Bodaboda wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wamelalamikia baadhi ya waendesha vyombo hiyo kuvujisha siri za wateja wao kwa watu wengine.
Wakizungumza na Vwawa Fm Radio April 15, 2025 wamesema tabia hiyo inaweza kuleta migogoro katika jamii hivyo kuwasihi kuheshimu kazi yao kama kazi nyingine za kuwaingizia kipato.
Kwa upande wao dereva bodaboda wamesema kuna baadhi ya madereva wanavujisha siri kutokana na abiria wao kukiuka makubaliano.
Mtaalamu wa masuala ya sheria Saduni Aizak amesema kuvujisha siri za mtu mwingine ni kosa la kisheria, akifafanua amesema.