Uyui FM
Uyui FM
2 July 2025, 12:11 pm

”Huitaji kujua mtu ametoka wapi au ni nani,akikukuta ofisini mhudumie” RC Chacha
Na Zabron George
Mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha, amewataka wakuu wa wilaya walioapishwa kufanya kazi kwa weledi na kutatua changamoto za wananchi bila ubaguzi.
Mkuu wa mkoa Chacha amesema hayo baada ya hafla ya uapisho kwa wakuu wa wilaya za Sikonge na Tabora katika ukumbi wa mtemi Isike Mwanakiyungi Manispaa ya Tabora.

Mkuu wa wilaya ya Tabora Upendo Wella na mkuu wa Wilaya ya Sikonge Thomas Myinga wameahidi kwenda kutatua kero za wananchi.

Katibu Tawala mkoa wa Tabora Daktari John Mboya amesema ili kazi ifanyike vizuri ni muhimu viongozi kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.