Unyanja FM
Unyanja FM
May 26, 2025, 12:49 pm

Wakati maeneo mengine wanamuona mamba kama mnyama mkali lakini sivyo kwa wilaya ya nyasa ambako baadhi ya sehemu amefanywa kitoweo na wahusika kufurahia ladha yake
Na Mussa ndonde
Hayo yameelezwa na wananchi wa kijiji cha nangombo kitongoji cha tembwe kinachopitiwa na mto luhekei unaomwaga maji yake maji yake kwenye ziwa nyasa.
Wamesema baadhi ya watu wilayani humo hutumia kama kitoweo huku wengine wakibainisha ladha ya nyama ya mnyama huyo.
JOSEPH MAHAYI ni mkazi wa kitongoji cha luhekei kwa upande wake amekiri watu wanatumia mamba kama kitoweo ila kuna taratibu ambazo zinafuatwa ili kukamilisha zoezi hilo.
MAHAYI amesema baada ya kumtega na kumkamata huitwa kiongozi wa kijiji kuthibitisha ukamatwaji wa mamba huyo na kumtoa nyongo ambayo husambalatishwa kwenye maji.
Tukio hilo hushuhudiwa na wananchi maana nyongo ni sumu na haipaswi kumilikiwa na mwanajamii
Pamoja na mamba kufanywa kitoweo wilayani nyasa wakazi waishio maeneo hayo hawajawai fanya nyama ya mamba kuwa biashara