Unyanja FM
Serikali yazidi kuimarisha miundombinu ya barabara na maji Nyasa
October 31, 2023, 10:43 am
Serikali yazidi kuimarisha miundombinu ya barabara na maji Nyasa
Mkuu wa wilaya ya nyasa MH.FILBERTO HASSAN SANGA amewahasa wananchi kutumia vizuri fursa za uchumi zinapojitokeza hasa kilimo na uvuvi kwa kuwa ndio shughuli tegemezi na zinazofanywa na watu wengi wilayani humo
aliyasema hayo oktoba 27 katika ziara yake alipotembelea kijiji cha lipingo kata ya lundo wilayani nyasa alipokuwa akipokea changamoto za wananchi wa kijiji hicho na wilaya kwa ujumla
katika hatua nyingine MH FILBERTO SANGA alisema serikali inaendelea na mikakati ya kuboresha miundombinu ya barabara pamoja na huduma za maji ili zimfike kila mwanachi na kuondokana na adha hiyo