Savvy FM
Savvy FM
2 Aprili 2026, 13:50

Jamii imeaswa kuacha kuwanyanyapa warahibu wa dawa za kulevya kwani kufanya hivyo hupelekea waathirika hao kushindwa kufikia huduma za matibabu.
Na Mariam Mallya
Afisa Kutoka mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevvya kanda ya kaskazini Brenda Mbati amesema familia zinapaswa kuwapokea na kuwasaidia warahibu kwa kuwatafutia matibabu badala ya kuwatenga.
Akizungumza na Savvy FM afisa huyo amesema Urahibu ni ugonjwa kama magonjwa mengine hivyo jamii haipaswi kutumia lugha za kuwanyanyapa kama kuwaita majina yasiofaa kama vile teja, chizi na mengineyo.
Arafa Ally ni miongoni mwa aliyewahi kuwa mrahibu wa dawa za kulevya amesema urahibu ulimuathiri kwa kiasi kikubwa na kupelea kupoteza familia yake .