Savvy FM

Meya Jiji la Arusha kukutana na mawakala wa uzoaji taka

January 4, 2026, 5:57 pm

Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranghe akiongea na wananchi wa Kata ya Sombetini.Picha na Mariam Mallya

Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranqhe, ametoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji kuandaa kikao maalum cha kukutana na mawakala wa uzoaji wa taka ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu usafi wa Jiji la Arusha.

Na Mariam Mallya

Maelekezo hayo yametolewa leo katika Kata ya Sombetini wakati wa muendelezo wa zoezi la ng’arisha Jiji la Arusha lililofanyika katika soko la Mbauda. Katika zoezi hilo, Meya Iranqhe alisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Halmashauri na mawakala wa uzoaji taka kwa lengo la kuhakikisha jiji linakuwa safi wakati wote.
Aidha, alielekeza kuwa utaratibu wa kupiga faini kwa wanaokiuka sheria za usafi uendelee kutekelezwa ipasavyo, sambamba na agizo la kutokufungua biashara kabla ya kufanya usafi katika maeneo yao ya kazi.

Sauti ya Maximilian Iranghe,Meya wa Jiji la Arusha

Kwa upande wake, Diwani wa Viti Maalum na Mratibu wa zoezi la ng’arisha Jiji la Arusha, Aminata Toure, aliwashukuru wananchi pamoja na wafanyabiashara waliojitokeza kushiriki zoezi hilo la usafi. Pia aliwahimiza kuendelea kuwa mabalozi wa usafi katika maeneo yao ili kudumisha mazingira safi na salama kwa jamii.

Sauti ya Aminata Toure,Diwani viti maalum na mratibu wa zoezi la usafi