Savvy FM
Savvy FM
December 15, 2025, 6:43 pm

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Jumatatu Disemba 15, 2025 amefungua na kuongoza Kikao cha kusikiliza kero na changamoto za bodaboda na Bajaji Mkoa wa Arusha, Kikao kilichofanyika kwenye Viwanja vya Makumbusho ya Azimio la Arusha.
Na Mariam Malya
Katika salamu zake za utangulizi, Mhe. Makalla aliyeambatana na Wakuu wote wa Wilaya za Mkoa wa Arusha, ameahidi na kuwahakikishia wananchi wa Mkoa wa Arusha kuwa utakuwa utamaduni wake mara zote katika Utumishi wake Mkoa wa Arusha kuwafikia na kuwasikiliza wananchi na Makundi mbalimbali ya Kijamii ili kuondoa kero zinazowakabili, akiagiza pia Wakuu wa Wilaya kufanya ziara za kuwatembelea, kuwasikiliza na kutatua kero za wananchi.
Kwa upande wa makatibu usafirishaji bodaboda na bajaji mkoa wa Arusha wameiomba serikali ya mkoa kuweza kuwatengenezea mazingira rafiki iliwaweze kutekeleza majukumu Yao ya usafirishaji