Savvy FM
Savvy FM
November 27, 2025, 6:01 pm

Janga la kupungua kwa mnyama kazi punda limezidi kuongezeka nchini Tanzania, huku ikikadiriwa kuwa takribani punda 150 wanavushwa na kuchinjwa kila mwezi kinyume na taratibu, na kuuzwa katika maeneo mbalimbali nje ya nchi. Hali hii imeibua wasiwasi mkubwa kwa wadau wa ustawi wa wanyama.
Na Mariam Malya
Akizungumza katika mkutano huo, Afisa Elimu wa Ustawi wa Wanyama, Bi. Diana Gladness Msemo, alisema takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ina makadirio ya punda wasiopungua laki tano, na idadi hiyo inaendelea kupungua kutokana na ukatili na uvunaji holela. Amefafanua kuwa uelewa mdogo wa sheria, kanuni na haki za wanyama umechangia sana kuongezeka kwa vitendo vya uvunjifu wa haki za punda nchini.
Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka ASPA, Bw. Albert Mbwambo, alieleza kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakiwateka na kuwachinja punda kwa madai ya kitoweo, huku wengine wakichuna ngozi na kuuza katika masoko ya ndani na nje ya nchi. Kitendo hicho kimetajwa kuwa kinyume na sheria za ustawi wa wanyama na kinaweza kusababisha kutoweka kwa mnyama huyo muhimu kwa jamii na shughuli za uzalishaji.