Savvy FM

Nasimama na Mama Tanzania kuwanufaisha wananchi Arusha

October 3, 2025, 3:33 pm

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Joseph Mkude akiongea na wananchi wa Arusha.Picha na Mussa Kinkaya

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Joseph Modest Mkude amezindua rasmi taasisi isiyo ya kiserikali ya Nasimama na Mama Tanzania yenye lengo la kumuunga mkono Rais dk Samia Suluhu Hassan Katika kila analolifanya pamoja pia na kuwakwamua vijana na kina mama kiuchumi.

Na Mussa Kinkaya

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya Joseph Mkude amewapongeza waanzilishi wa Nasimama na Mama Tanzania kwa kuwa na wazo hilo lenye lengo la kuisaidia Serikali na kusema kuwa wao kama Serikali watakuwa nao bega kwa bega kuwaunga mkono.

Sauti ya Joseph Modest Mkude,Mkuu wa wilaya ya Arusha

Akisoma taarifa ya taasisi hiyo katibu mkuu wa Nasimama na Mama Tanzania Kanda ya Kaskazini ndugu Dionis moyo amesema wataandaa mafunzo ya miezi mitatu kwaajili ya waandishi wa habari mkoani Arusha kwa lengo la kujifunza kuhusu utalii na kuandika habari za utalii kwa kushirikiana na TANAPA

Sauti ya Dionis Moyo,Katibu Mkuu Nasimama na Mama Tanzania Kanda ya Kaskazini

Mwekeiti wa taasisi hiyo Kanda ya Kaskazini Monica Selemani ameeleza kuwa lengo la taasisi hiyo ni kuhakikisha kuwa wanawasaidia vijana kujikwamua kiuchumi wakizingatia katika sekta ya kilimo na ufugaji

Sauti ya Monica Selemani,Mwenyekiti Nasimama na Mama Tanzania Kanda ya Kaskazini

Afisa muhifadhi mkuu kutoka TANAPA amewataka wananchi kuanza kufanya utalii wa ndani na kuacha dhana kuwa utalii ni kwa ajili ya wageni pekee.

‎Amesema kufanya utalii wa ndani kutasaidia Serikali kuongeza kipato na kufanya shughuli nyingi za maendeleo ya wananchi.

‎Amesema wao kama shirika wataendelea kusimama na taasisi hiyo ya Nasimama na Mama Tanzania katika kuunga mkono juhudi za Serikali chini ya Rais Dk Samia Suluhu kutangaza utalii na kuendelea kuongeza pato la Serikali.

Sauti ya Afisa muhifadhi mkuu kutoka TANAPA