Savvy FM

Wananchi waonesha mshikamano, uadilifu kwa wateule wa udiwani jijini Arusha

August 20, 2025, 12:38 pm

Wananchi na wagombea udiwani wakielekea ofisi za Kata kuchukua fomu.Picha na Jenipha Lazaro

Mamia ya wananchi kutoka kata za Sakina na Ungalimited jijini Arusha, leo wamejitokeza kwa wingi kuwasindikiza madiwani wao kuchukua fomu za kugombea nafasi ya udiwani kupitia chama cha Mapinduzi, kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Na Jenipha Lazaro

Wakizungumza na Savvy FM, wananchi hao wamesema wameamua kuonyesha mshikamano wao kwa viongozi waliowatumikia kwa uadilifu na kwa mafanikio.

Sauti ya Wananchi wa Kata za Sakina na Ungalimited

Kwa upande wao, wagombea udiwani, Hilary Molel wa Kata ya Sakina na Mahamud Said Omar wa Kata ya Ungalimited, wamewashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono, wakisema kuwa uungwaji huo wa mkono ni uthibitisho kuwa bado wana deni kubwa kwa wananchi wao

Sauti ya wagombea udiwani Kata ya Sakina na Ungalimited