Savvy FM

Shimo la maji taka linavyokwamisha biashara ya maafisa usafirishaji Arusha

August 18, 2025, 8:53 pm

Maafisa usafirishaji jijini Arusha wakiwa kwenye majukumu yao ya kazi.Picha na Jenipha Lazaro

Maafisa usafirishaji maarufu waendesha bodaboda kutoka kijiwe cha Mnazi Mmoja, mtaa wa Mjini Kati jijini Arusha, wameiomba serikali na mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto ya shimo linalotuamisha maji machafu na taka, ambalo limekuwa kero kubwa kwao na kuwazuia kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Na Jenipha Lazaro

Wakizungumza na Savvy FM mapema leo, baadhi ya waendesha bodaboda akiwemo Shauri Abdalah, Lukas Njau na Filber Laurent wamesema kuwa licha ya kutoa malalamiko yao kwa mamlaka mbalimbali, bado tatizo hilo limeendelea kuwa sugu.

Sauti ya Maafisa usafirishaji Jiji la Arusha

Kwa upande mwingine, Mfaume Abdi – Katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kati, pamoja na mdau wa maendeleo wa eneo hilo Jumapili Abdi, wamekiri kuwepo kwa changamoto hiyo.

Sauti ya Mfaume Abdi na Jumapili Abdi