Savvy FM

Serikali yatoa msamaha ushuru wa forodha kwa malighafi

August 13, 2025, 3:18 pm

‎Meneja wa TRA mkoa wa Arusha, Deogratius Shuma. Picha na Jenipha Lazaro

Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA, imeamua kutoa msamaha wa ushuru kwa malighafi zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, ikiwa ni hatua ya kuimarisha uzalishaji wa bidhaa ndani ya nchi na kuweka usawa wa bei sokoni.

Na Jenipha Lazaro

Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Arusha, Deogratius Shuma, amesema kuwa serikali imeamua kutoa msamaha wa Ushuru wa Forodha (Duty Remission) kwa malighafi zinazoagizwa kutoka nje ya nchi ili kuwezesha viwanda vya ndani kuzalisha bidhaa kwa gharama nafuu, sambamba na kusababisha usawa wa bei sokoni hasa dhidi ya bidhaa zinazotoka nje.

Sauti ya Meneja wa TRA mkoa wa Arusha, Deogratius Shuma

‎Katika mafunzo yaliyotolewa kwa maafisa wa forodha, mawakala wa forodha pamoja na wazalishaji wa bidhaa, maafisa kutoka makao makuu ya idara ya forodha jijini Dar es Salaam wamesema mabadiliko hayo yamejikita kwenye sheria ya fedha ya mwaka 2025.‎

Sauti ya Hassan Minga, Afisa forodha

‎Hatua hii ya msamaha wa ushuru inatarajiwa kuimarisha viwanda vya ndani na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia bidhaa bora, nafuu na zenye ushindani katika soko la ndani na kanda ya Afrika Mashariki.‎‎