Savvy FM

Nyuki kutumika kufukuza tembo waharibifu

June 30, 2025, 11:57 pm

Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Dkt. Eblate Mjingo akizungumza na wanahabari. Picha na Gasper Sambweti

Serikali kutumia mizinga ya nyuki kukabiliana na tembo wavamizi na waharibifu wa mazao.

Na Gasper Sambweti

Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania TAWIRI iliyopo mkoani Arusha imeingia makubaliano ya miaka mitano na taasisi isiyo ya kiserikali ya Tembo Pilipili kwa lengo la kuisaidia jamii kupambana na tembo katika maeneo yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Dkt. Eblate Mjingo amesema wamejiwekea mikakati ya kubuni mbinu ya namna ya kupambana na tembo bila madhara kwa kutumia mizinga.

Sauti ya Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Dkt. Eblate Mjingo

Naye Mtafiti Mkuu wa TAWIRI, Wilfred Njama amesema mradi huu umekuja kwa wakati sahihi na wao watautumia kama fursa kwa kuweka mizinga zaidi ya 100 katika shamba darasa .

Sauti ya Mtafiti Mkuu wa TAWIRI Wilfred Njama

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tembo Pilipili Alex Chang’a amesema wapo tayari kutoa elimu katika maeneo mbalimbali lengo likiwa ni kuifikia jamii na kujifunza namna gani wanaweza kutumia nyuki kuwafukuza tembo waharibifu.

Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tembo Pilipili Alex Chang’a