Savvy FM
Savvy FM
June 18, 2025, 5:25 pm

“Mipango ya ujenzi na miradi inayoendelea hii Makonda hakujanayo ni miradi ilikuwepo ili soko lilipaswa kujengwa na pesa ilitolewa toka 2021 shilingi millioni 500 pesa zimekaa kwenye akaunti”.
Na Mariam Mallya
Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda ameongoza mamia ya wananchi wa jiji la Arusha kushuhudia hafla ya utiaji saini ujenzi wa Soko la Machinga (Machinga Business Park) eneo la Morombo na uwanja wa mpira wa Arusha City Club katika kata ya Murieti, Jiji la Arusha.
RC Paul Makonda ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo mkoani Arusha.
Akiwasilisha taarifa za mradi wa uwanja wa mpira wa Arusha city kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Nindwa Maduhu amesema uwanja huo utajengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 9.6 na utakuwa na uwezo wa kubeba watazamaji 8,000 waliokaa.