Savvy FM
Savvy FM
June 7, 2025, 7:00 pm

Wananchi wa kijiji cha Mti mmoja wamepoteza matumaini yao ya utatuzi wa mgogoro wa ardhi baina ya mtu binafsi na eneo la malisho maarufu Sepeko baada ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli kutoonekana katika eneo la mgogoro kama alivyoahidi.
Na Juliana Laizer
Hii inakuja mara baada ya mkutano ulofanyika tarehe 22 mwezi jana baina ya wananchi na wataalamu wa ardhi kutoka wilayani ambapo baada ya malalamiko yao kutopata suluhu ndipo Savvy FM ikamtafuta Mkuu wa Wilaya ya Monduli Festo Kiswaga na baadaye kutangaza tarehe nne mwezi huu kuwa ndio siku ya kutatua mgogoro huo ambapo hali haikuwa sawa baada ya kutoonekana na wananchi kuamua kufanya mkutano wao wenyewe bila uongozi wowote na kuweka agenda moja ya namna ya kuikomboa ardhi hiyo ya malisho yenye hekari 85 inayodaiwa kuporwa na mtu mmoja.
Baada ya malalamiko hayo tulijitahidi kumtafuta Mkuu wa Wilaya ya Monduli ndugu Festo Kiswaga na juhudi zetu hazikufanikiwa ndipo tukamtafuta Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Mti mmoja Ibrahimu Leoyo ambapo amejibu kuwa yeye hajui kama kuna mgogoro wowote bali ni watu wameamua kumchafua.