Savvy FM
Savvy FM
June 2, 2025, 2:43 pm

Wananchi wa kijiji cha Engutukoit kata ya Oldonyowas wametoa siku 7 kupasua chungu kwa ajili ya watu wote wanaotaka kuwapora eneo la ardhi kwa ajili ya malisho ya mifugo yao.
Na Juliana Laizer
Wakizungumza katika mkutano ambao mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ambaye aliwakilishwa na Naibu Katibu Tawala wa Arumeru Bw. Japhet Nguirana wenyeviti wa vijijiji hivyo wameleza kuwa serikali ya kijiji kupitia Mtendaji wamefoji muktasari wa uongo ambao lengo ni kuwapora ardhi kwa ajili ya malisho.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Engutukoit Loserian Paangu ameiomba serikali kutatua tatizo hilo la mgogoro wa ardhi ili wananchi wake wasiendelee kuteseka
Kutokana na sintofahamu hiyo mgeni rasmi ndugu Japhet Nguirana ambaye ni Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru amewashukuru kwa kikao na kuahidi kuyafikisha malalamiko yao kwa Mkuu wa Wilaya.