Savvy FM
Savvy FM
May 27, 2025, 12:10 pm

Wawekezaji wa utalii katika bonde la mto wa Mbu wilayani Monduli wametakiwa kufuata sheria na taratibu za kiuwekezaji na kuepuka kujimilikisha maeneo yalio chini ya wananchi au vijiji bila kuwashirikisha kisheria.
Na Juliana Lizer
Onyo hilo limetolewa na mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Festo Kiswaga wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Majengo(Mto wa Mbu) baada ya kutokea sintofahamu katika mikataba iliyosainiwa kati ya viongozi wa kijiji cha Migombani na mwekezaji aliyejulikana kwa jina la Professor Baltazari.
Amesema viongozi wa kijiji ambao ni mwenyekiti pamoja na mtendaji wamehusika kumuongezea mwekezaji huyo mkataba halali wa miaka 15 hadi miaka 33 na kumkabidhi hatimiliki ya miaka 99 bila kufuata sheria ya kuwashirikisha wananchi jambo alilolitaja kuwa ni kinyume na taratibu za nchi.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Migombani kwa pamoja wameishukuru serikali chini ya mkuu wa Wilaya Festo Kiswaga kwa kuendelea kufuatilia swala hilo na kutoa majibu kwani hawakuwai kunufaika na wawekezaji hao katika maeneo yao.