Savvy FM
Savvy FM
April 30, 2025, 5:47 pm

Shirika la soil for the feature linalojishughulisha na biashara ya hewa ukaa limewasafirisha baadhi ya wananchi na viongozi wa vijiji na kata katika Wilaya za Monduli na Longido hadi Kajiado nchini Kenya ili kupatiwa elimu ya namna ya biashara hiyo inavyofanyika katika nyanda za malisho.
Na Juliana Lizer
Wakizungumza mara baada ya mafunzo hayo wananchi hao wamesema walichojifunza na kujionea zaidi ni namna uvunaji wa hewa ukaa unavyofanyika katika nyanda za malisho bila kuathiri kitu chochote
Lekoko Ngotiek ni mratibu wa mradi wa carbon wilayani Monduli amezungumzia makubaliano waliyokubaliana na jamii ya kimasai hadi kupelekea kuwapeleka nchini Kenya kupata elimu juu ya hewa ukaa