Savvy FM
Savvy FM
April 23, 2025, 10:37 am

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Doto Biteko amewasili mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya kikazi ambapo atakagua miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya maji .
Na Mwandishi Wetu
Akizungumza na wananchi wilayani Monduli wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji kijiji cha Esilalei, Dkt.Biteko amewataka kutunza vyanzo vya maji wanavyoletewa na serikali ili viweze kudumu na kutumika na vizazi vijavyo.
Aidha amewasihi wananchi kuendelea kudumisha amani na kuepuka kugawanywa katika makundi ya kidini ama kikabila katika kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu na kuwataka kuzingati kuchagua viongozi wenye sifa na uwezo.