Radio Kwizera
Radio Kwizera
August 23, 2025, 3:42 pm

Katika ziara ya kusikiliza na kutatua kero DC Nkinda alipokea malalamiko kutoka kwa mwananchi Emanuel Maduhu ambaye anadai aliuziwa kiwanja na serikali ya mtaa huo ambacho kilikuwa kimeuzwa awali.
Na Samuel Samsoni- Kahama
Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Frank Nkinda ameagiza hatua za kisheria zichukuliwe kwa aliyekuwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Igomelo, kata ya Malunga Manispaa ya Kahama mkoani humo Laurent Benedicto endapo atabainika kuwa na hatia kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka kipindi alipokuwa kiongozi ikiwemo kuuza viwanja mara mbili.
Taarifa zaidi inaripotiwa na Samuel Samsoni kupitia kipindi cha yaliyojiri
Sauti ya Samuel Samson akiripoti kuhusu tukio hilo lililojiri kwenye ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Frank Nkinda wakati wa kusikiliza kero mbalimbali