Radio Kwizera

DC Biharamulo afunga mafunzo ya jeshi la akiba

August 23, 2025, 3:17 pm

Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, SACP Advera John Bulimba akizungumza wakati wa kufunga hafla ya kufunga Mafunzo ya 21 ya Jeshi la Akiba (Mgambo) kwa mwaka 2025. Picha William Mpanju

DC Bulimba amewapongeza kwa kuhitimu kwa nidhamu, umakini na utayari, akiwataka wakawe mfano bora kwa jamii na kutumia mafunzo waliyopata kwa kuhudumia wananchi na kulinda usalama wa jamii.

Na William Mpanju- Biharamulo, Kagera

Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, SACP Advera Bulimba, ameongoza hafla ya kufunga Mafunzo ya 21 ya Jeshi la Akiba (Mgambo) kwa mwaka 2025 na kutoa onyo kali kwa viongozi wa vijiji na kata kutowadhalilisha askari wa jeshi la akiba.

SACP Bulimba aliwataka viongozi na wananchi kwa ujumla kuwaheshimu na kuwashirikisha askari hao akisisitiza kuwa ni sehemu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na wanapaswa kutumika kikamilifu katika kudumisha amani na usalama wa jamii.

Aidha, alitoa onyo kali kwa viongozi watakaojaribu kugomesha mafunzo ya jeshi la akiba, akibainisha kuwa hatua hizo zitachukuliwa kama kukaidi agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ameanzisha mafunzo hayo kwa lengo la kuandaa vijana kuwa wazalendo na walinzi wa nchi yao.

Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, SACP Advera Bulimba akikagua gwaride wakati wa kufunga hafla ya kufunga Mafunzo ya 21 ya Jeshi la Akiba (Mgambo) kwa mwaka 2025. Picha William Mpanju

Akihutubia wahitimu, DC Bulimba amewapongeza kwa kuhitimu kwa nidhamu, umakini na utayari, akiwataka kwakawe mfano bora kwa jamii na kutumia mafunzo waliyopata kwa kuhudumia wananchi na kulinda usalama wa jamii.

Undani wa taarifa hii anaripoti William Mpanju kutoka Biharamulo kupitia kipindi cha YALIYOJIRI

Sauti ya William Mpanju akiripoti zaidi kuhusu hafla ya kufunga Mafunzo ya 21 ya Jeshi la Akiba (Mgambo) kwa mwaka 2025