Radio Kwizera

Doria ya siku 12 yadaka Wahamiaji haramu 793

August 4, 2025, 8:08 pm

Raia wa kigeni wakiwa katika Ofisi za Uhamiaji mkoani Kigoma baada ya kukamatwa nchini walipoingia pasipo kufuata sheria. Picha Naomi Milton

Raia hao waliokamatwa ni kutoka mataifa matano ambayo ni Burundi, DR Congo, Rwanda, Uganda na Tanzania.

Na Naomi Milton- Kigoma

Takribani wahamiaji haramu 793 wamekamatwa na Idara ya Uhamiaji mkoani Kigoma kwa kipindi cha siku 12 katika doria na misako inayoendelea huku lengo ikiwa ni kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inaimarika husuni kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Afisa Uhamiaji mkoani Kigoma Dominick Kibuga imeeleza kuwa raia hao ni kutoka mataifa matano ambayo ni Burundi, DR Congo, Rwanda, Uganda na Tanzania.

Kaimu Afisa Uhamiaji mkoani Kigoma Dominick Kibuga akieleza utaratibu wa raia wa kigeni kuingia nchini.
Raia wa kigeni wakiwa katika Ofisi za Uhamiaji mkoani Kigoma baada ya kukamatwa nchini walipoingia pasipo kufuata sheria. Picha Naomi Milton

Aidha amesema hatua zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na baadhi wamerejeshwa nchini kwao na wengine kufikishwa mahakamani huku wengine wakiachiwa huru baada ya uchunguzi

Raia wa kigeni wakiwa katika Ofisi za Uhamiaji mkoani Kigoma baada ya kukamatwa nchini walipoingia pasipo kufuata sheria. Picha Naomi Milton