Mradi wa umeme maporomoko ya Rusumo kuzinduliwa Disemba
September 30, 2023, 8:18 pm
Mradi huo wa umeme uliopo Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda utazinufaisha nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi.
Na, Laurent Gervas
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Mashaka Biteko amesema mradi wa kufua umeme wa maporomoko ya Rusumo utazinduliwa rasmi Disemba mwaka huu 2023 ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa Tanzania, Rwanda na Burundi
Amesema hayo leo akiwa na mawaziri wenzake ambao ni Waziri wa Miundombinu wa Rwanda Dkt. Jimmy Gasore na waziri wa Nishati na Madini wa Burundi Mhandisi Ibrahim Uwizeye katika eneo la mradi wa kufua umeme wa maporomoko ya Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera baada ya kuwasha mtambo mmoja.
Amesema ujenzi wa mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 99.7 nakwamba mpaka kufikia mwezi Oktoba mwaka huu mashine zote 3 zitakuwa zimewashwa, hivyo kukamilika kwake utakuwa mwarobaini wa matatizo ya umeme katika ukanda huu wa nchi hizi tatu.
Aidha Waziri Biteko amewataka wananchi wa Tanzania, Rwanda na Burundi kushirikiana na serikali zote 3 kuulinda mradi huo.