Idara ya afya Wilayani Ngara Mkoani Kagera leo imezindua zoezi la utoaji chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 8.
September 21, 2023, 1:13 pm
Katibu tawala wa Wilaya ya Ngara Bw.Jawadu Yusufu aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera akizindua zoezi la kutoa chanjo ya Polio kwa watoto chini ya umri wa miaka 8 katika hospitali ya wilaya Nyamiaga.
Idara ya afya Wilayani Ngara Mkoani Kagera leo imezindua zoezi la utoaji chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 8 ili kuwaepusha kupata ulemavu ambao unakingika kwa kutumia chanjo hiyo.
Na Godwin Bruchard:
Idara ya afya Wilayani Ngara Mkoani Kagera leo imezindua zoezi la utoaji chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 8 ili kuwaepusha kupata ulemavu ambao unakingika kwa kutumia chanjo hiyo.
Uzinduzi huo umefanyika katika Hospitali ya Wilaya Nyamiga ambapo umeudhuriwa na viongozi wa vitongoj, vijiji na kata ili kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo kaimu katibu tawala wa Wilaya ya Ngara Bw.Jawadu Yusufu aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo amesema kuwa chanjo hiyo inalenga kupunguza vifo kwa watoto na ulemavu wa kudumu.
Katibu tawala wa Wilaya ya Ngara Bw.Jawadu Yusufu aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera akimuwekea alama mtoto baada ya kupata chanjo ya polio katika uzinduzi wa zoezi la kutoa chanjo ya Polio kwa watoto chini ya umri wa miaka 8 katika hospitali ya wilaya Nyamiaga.
Katika hatua nyingine Mratibu wa chanjo Wilaya ya Ngara Bw.Yunusi Himid amesema kuwa zoezi hilo litafanyika kwa muda wa siku nne ambapo jumla ya watoto elfu 93 na 830 wanatarajiwa kupatiwa chanjo hiyo.