Waandishi watajwa kuwa silaha, chachu mabadiliko ya maendeleo kwenye jamii
July 4, 2023, 11:37 am
Waandishi wa habari nchini Tanzania wametakiwa kuzipa nguvu habari zinazopatikana katika jamii inayowazunguka ili kuleta mabadiliko chanya kimaendeleo kwa Watanzania
Na; Pascal Mwalyenga
Waandishi wa habari nchini Tanzania wametakiwa kuzipa nguvu habari zinazopatikana katika jamii inayowazunguka ili kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa watanzania
Kauli hiyo imetolewa na mkufunzi kutoka TADIO Amua Rushita katika mafunzo yanayoendelea ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka redio za jamii juu ya namna ya kuchapisha habari katika jukwaa la Radio Portal.
Amesema kupitia jukwaa la Radio Portal wanaendelea kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka Radio za kijamii washirika 35 ili kuwa na uwezo kuandika habari kwa usahihi kwa kufuata misingi ya kihariri ili kuinufaisha jamii
Kupitia jukwaa la Radio Portal tunanaendelea kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka Radio za kijamii washirika 35 ili kuwa na uwezo kuandika habari kwa usahihi kwa kufuata misingi ya kihariri ili kuinufaisha jamii
Kwaupande wake Hilali Ruhundwa mkufunzi na mhariri wa Radio Portal kutoka TADIO amesema mwandishi anapaswa kujikita katika habari za uchunguzi ili kumjenga katika ukomavu wa tasnia ya habari na kuisaidia jamii.
Nao baadhi ya waandishi wanaoshiriki katika mafunzo hayo yanayoendelea katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza wasema mafunzo hayo yanawasaidia kuwajenga kuandika habari zinazoigusa jamii na kuwavutia wasomaji.