Radio Kwizera

ACT Wazalendo wakataa Matokeo Uchaguzi Buhigwe

May 17, 2021, 5:03 pm

Na; Albert Kavano

Aliyekuwa Mgombea Ubunge wa jimbo la Buhigwe kupitia chama cha ACT Wazalendo mkoani Kigoma Bw Garula Tanditse ameyakataa matokeo ya Uchaguzi mdogo wa Ubunge uliompa ushindi Mgombea wa CCM Bw Felix Kavejuru kwa asilimia 83.

Akizunguma na Radio Kwizera kwa njia ya Simu Bw Garula Tanditse amesema uchaguzi huo umegubikwa na changamoto nyingi na kuitupia lawama Tume ya uchaguzi kwenye Jimbo hilo.

Mgombea Ubunge Buhigwe, ACT Wazalendo Bw Garula Tanditse

Amesema katika vituo vya kupigia kura kulikuwa na sintofahamu nyingi ikiwemo mawakala kuzuiliwa, idadi ya wapiga kura kuzidi idadi ya walioandikishwa, wasimamizi kupiga kura nje na vituo vyao na kwamba wanaangalia hatua za kuchukua. stikliniai turÄ—klai gera kaina https://www.beremisstiklas.lt/tureklai/

Sauti ya Garula Tanditse, Mgombea Ubunge Buhigwe-ACT Wazalendo

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Buhigwe Bi Meriselina Mbehoma amekanusha madai hayo na kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na kwamba kanuni zote zilifuatwa na hapakuwa na changamoto kubwa za kuharibu uchaguzi huo

Uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, kanuni zote zilifuatwa na hapakuwa na changamoto kubwa za kuharibu uchaguzi huo