Radio Kwizera

Wafanyabiashara Kigoma wana imani na Dr Mpango

March 30, 2021, 6:47 pm

Na; Phillemon Golkanus

Wafanyabiashara mkoani Kigoma wamesema wana imani kubwa na Makamu wa Rais Mteule Dr Phillip Mpango hata kabla ya kuteuliwa katika wadhifa huo mpya

Wafanyabiashara (Picha kutoka Maktaba)

Wafanyabiashara hao wamesema Dr Mpango ni kiongozi mwenye maono na mipango mikubwa ya kukuza uchumi wa taifa hata wakati akiwa Waziri wa Fedha na Mipango

Katibu wa Chama cha Wafanyabiashara, wenye viwanda na wakulima, TCCIA mkoani Kigoma Bw Prosper Guga amesema wafanyabiashara wa mkoa huo hawana shaka na uteuzi huo kwa kuwa tangu awali amekuwa mtetezi wao katika shughuli zao