Radio Kwizera

Mwanafunzi afariki akiimba Kwaya, Biharamulo

March 30, 2021, 5:48 pm

Na; William Mpanju

Mwanafunzi Samson Nditiye wa Darasa la 7 katika shule ya msingi Nyakanazi wilayani Biharamulo mkoani Kagera amefariki baada ya kuangukiwa na ukuta akifanya mazoezi ya kwaya huku wengine 6 wakijeruhiwa kufuatia mvua iliyoambatana na upepo mkali

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyakanazi BwJackson Julius amesema hayo wakati akitoa taarifa kwenye kamati ya ulinzi na usalama iliyoongozwa na Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, Kanali Mathias Kahabi pamoja na kamati ya maafa ya wilaya hiyo

Amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na moja jioni wakati mvua iliyoambatana na upepo mkali ikinyesha na kwamba pamoja na kifo hicho, pia nyumba 38 zimeanguka yakiwemo makanisa matatu

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama wilayani Biharamulo Kanali Mathias Kahabi amesema baada ya kutembelea kanisa lililoanguka na kusababisha kifo cha Mwanafunzi huyo amebaini kuwa kanisa hilo lilijengwa chini ya kiwango

DC Biharamulo, Kanali Kahabi akielezea kifo cha Mwanafunzi wa Darasa la Saba