Mtegani FM

SUZA watoa mwanga kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne

23 July 2025, 2:48 pm

Picha ikionesha Afisa Udahili kutoka chuo kikuu cha Zanzibar Suza kushoto ni ndugu haji kassim haji na kulia ni Ali Shauri jecha, wakiwa katika studio ya Mtegani FM, Picha na Miraji Manzi Kae.

Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kimefungua rasmi nafasi za masomo kwa msimu wa 2025/2026 huku kikiwapa kipaombele wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na kufaulu kwa walau alama D 4.

Na Miraji Manzi Kae

Msimu wa masomo wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kwa mwaka 2025/2026 umefunguliwa rasmi siku ya leo Julai 23 na Afisa Udahili Ndg. Haji Kassim Haji pamoja na Ali Shauri Jecha katika studio za Mtegani FM, ambapo wamesema nafasi za kujiandikisha zipo wazi kuanzia sasa na wamepewa kipaombele zaidi wanafunzi waliomaliza kidato cha nne walio na ufaulu wa angalau D 4 katika masomo yao.

Ameongezea kusema kuwa lengo la ufunguzi wa masomo ya msimu huu na kujiandikisha kupitia redio jamii ni kuwapa nafasi watu walio vijijini kwa ukaribu zaidi na chuo hicho, pia wanapokea watu wa aina tofauti katika chuo hicho kwa ajili ya kujiunga.

Sambamba na hayo ameorodhesha kozi mbalimbali zinazofundishwa katika chuo hicho ikiwemo uandishi wa habari, hotel management nk kuanzia ngazi ya cheti na ngazi zote kwa ujumla.

Sauti ya Afisa Udahili Ndg. Haji Kassim Haji.