Bunda FM Radio
Bunda FM Radio
August 7, 2025, 7:19 pm

‘‘Mtoto anatakiwa kujisikia huru na salama wakati wa unyonyeshaji kwa kupewa ushirikiano na sio mama unanyonyesha huku unachati mtandaoni unasahau zoezi la kumnyonyesha Mtoto” Grace martin Afisa lishe mkoa wa Mara
Na Amos Marwa
Jamii mkoa wa Mara imeaswa kutengeneza mazingira wezeshi kwa Mama anaenyonyesha ili kukuza na kulinda haki za wanawake kunyonyesha popote na wakati wowote.
Hayo yamebainishwa na Afisa lishe mkoa wa Mara Grace Martin wakati akizungumza na Bunda FM katika kipindi cha Busati la Habari ikiwa ni siku ya kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji iliyoanza agosti mosi hadi agosti 7. Ameongeza kuwa suala la unyonyeshaji si la mama pekee bali ni la jamii nzima akiwemo Baba na wote wanaomzunguka Mama.