Buha FM Radio
Buha FM Radio
25/02/2026, 19:01

“Watoto wamefikia sehemu wanajichukulia maamuzi yao jambo linalosababisha kuzalisha majambazi, vibaka, watoto wa mtaani jambo ambalo sio zuri na sisi kama ustawi wa jamii tunaendelea kutoa elimu katika jamii na kuwasisitiza kushirikiana katika malezi” Virginia Fredinand.
Na; Emily Adam
Baadhi ya wazazi katika Wilaya ya Kasulu wametaja sababu zinazopelekea kushindwa kushirikiana katika malezi ya watoto jambo lilalopelekea mmomonyoko wa maadili kwa kizazi kilichopo na kijajcho.
Kwa muujibu wa Majapisho mbalimbali Ulimwengu likiwemo chapisho la Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu imeeleza jinsi jamii ilivyo na mchango mkubwa katika malezi ya watoto Makala ya kipindi chetu leo imeelaza kinaga ubaga jinsi Jamii inavyopaswa kushiriki katika malezi ya watoto.