Buha FM Radio

Madiwani Kasulu waagizwa kusimamia bima ya afya kwa wote

January 29, 2026, 12:07 am

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu wakiwa katika ukumbi wa Kigoma katika Halmashauri hiyo. Picha na Sharifat Shinji.

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu wamehimizwa kusimamia maswala yote ya maendeleo ikiwemo swala la Bima ya afy kwa wote.

Na; Sharifat Shinji

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mhe. Balozi Simon Sirro, amewaagiza madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kuwahimiza wananchi katika maeneo yao kuhakikisha wanajisajili katika mpango wa Bima ya afya kwa Wote.

Maagizo hayo ameyatoa wakati wa kikao cha Robo ya Pili cha Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu ambapo amesema dirisha la usajili limeshafunguliwa kwa Mkoa wa Kigoma kwa kundi la watu wasiojiweza, ambapo serikali imeshatenga shilingi bilioni 4.9 na kuwasisitiza madiwani kusimamia jukumu la kuwapa elimu ya uelewa juu ya Bima hiyo.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Balozi Simon Sirro.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mhe. Balozi Simon Sirro. Picha na Sharifat Shinji.

 Aidha Siro amewasihi madiwani wanasimamia na kufuata sheria na kuwasaidia wananchi katika utekelezaji wa majuku yao bila kuvunja sheria na miongozo inayowaongoza katika maeneo yao.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Balozi Simon Sirro.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Mhe. Charles Kadogo, akifunga Kikao cha Robo ya Pili cha Baraza la Madiwani, ambapo amesisitiza umuhimu wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya madiwani na watendaji wa Serikali katika ngazi zote kwa ajili ya utekelezaji bora wa majukumu ya maendeleo kama ilivyoelekezwa na Mkuu wa Mkoa.

Sauti ya mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Mhe. Charles Kadogo.